Thursday, January 29, 2009

Ukisikia mkonge ndio huu!!!

Kama inavyoonekana pichani, mkonge wa moja ya gari za kazi Land Cruiser ukiwa umechomewa kwa lengo kuubwa la kupambana na vibaka. Inasemekana gari kama hiyo pindi (Mfano) ipatapo ajali wale wapenda kung'oa vifaa hukimbilia huo mkonge. Habari zinasema kwamba unagharama kuubwa sana ndio sababu ya vibaka kuwinda ulaji huo wanaojua/fahamu magari wanaelewa hilo.

Haya ndio mamboz ya vijijini (Biashara matangazo)


Ufahamu!!

Taa hii inatumia nishati ya umeme wa jua kwa kidhungu Solar power, pamoja na udogo wake inatoa mwanga wa kutosha kama tubelight tulizozizoea majumbani na kwingineko

Football ground.

Pichani unauona uzio ambao upende wa pili kuna mechi ikiendelea wakati picha hii inachukuliwa, kiingilio ndio kitachokuwezesha kujua ya upande wa pili.

Kama mweleka vile...!

Unaweza ukajua nini kimeikumba pikipiki hii?

Kijijini nako kweeema kabisa!

Na njiwa nae yupo kutafuta chakula pichani.

Kwa wengine hili ni "deal" au sio?


Kwenda kwa Rais mstaafu awamu ya tatu...

Unatambaa na mkeka saafi kabisa kwenda kijijini Lupaso (Masasi-Mtwara)
Kituo cha afya kijijini Lupaso hakipo nyuma.

Majengo ya Kitua hicho cha afya Lupaso karibu kabisa na kwa Mheshimiwa rais Mstaafu.



Enzi hizi hata mimi nilipita!!


Nauli!

Inasemekana kuwa kwa baadhi ya magari almaarufu makenta ama malori yabebayo abiria yanayofanya safari zake kwenda Tunduru kupitia njia ya Mtwara wanawake ndio hulipa nauli kubwa, hili nikauliza na kujibiwa kuwa baadhi ya makenta/malori hayo ni vimeo (Mabovu) hivyo linapohitaji msaada wa kulisumkuma liwake wanaume ndio wanashughulika. Swali je kwa mwanaume akitaka kulipa nauli kubwa kidogo na yeye atakubaliwa?