Monday, February 9, 2009

Soma hii

Ni habari ya kweli sio hadithi: Ilitokea siku moja wanakijiji walimpeleka mgonjwa wao zahanati ya kijiji. Walipofika zahanati kwa sababu mgonjwa wao alikuwa anaumwa sana wakaandikiwa rufaa ya kwenda katika hospitali ya rufaa (wilayani). Cha kuchekesha na kusikitisha baadhi ya wauguzi (wanakijiji) wa mgonjwa huyo wakamletea mganga wa zahanati hiyo jogoo ili awaahirishie safari ya kwenda hospitali ya wilaya. Yule mganga alishikwa na butwaa na kuwashangaa sana bila majibu. Mganga msimamo wake ulibakia pale pale, alibaki kuwauliza kuthamini utu na huyo jogoo je walifikiria mara mbili au?
Hivi ni vijimambo vya vijijini.

Pweza

Kaka pichani akimtayarisha pweza kwa kumpigapiga ili nyama iwe laini.

Juu ya mawe!


Safari na mziki!

Kwa wenzako ni kawaida tu hili. Hapo wanavuka kwenda upande wa pili panaitwa Msangamkuu (Mtwara).
Abiria wakisheheni kuvuka bahari.


Promotion promotion!


Ardhi na utajiri wa Tanzania.

Kama arhi tunayo ya kutoosha nini kingine tupewe?

Mkeka...

Panapo dharula ndege ndogo haitui hapo?

Afya mbele mengine baadae

Pichani kina mama wakingojea kupata tiba/ushauri nk kwa afya za watoto wao.

Ni Jahazi au Mtumbwi?

Binafsi nilijichanganya na kutotambua kama haya niyaonayo ni majahazi au mitumbiwi?
Nisaidie jibu kwa kura yako ya maoni ya jimbo la baharini.

Unawajua Flamingo?