Friday, April 24, 2009

Wacheza ngoma siku ya malaria!

Ming'oko nayo iliwepo siku ya uzinduzi Malaria Day


Uzinduzi rasmi wa Malaria Day 23/4/2009



Maadhimisho haya ya siku ya malaria duniani yamezinduliwa rasmi jana tarehe 23 April 2009 na Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Mstaafu Anatoli Tarimo. Mwenye kaunda suti ya Khaki. Wakazi wa mtwara watapata pia fursa ya kumuona Balozi wa Malaria Ivyone Chakachaka akiambatana na Mkongwe Lady JD. Patakuwa hapatoshi kwa wakazi wa mji huu.


Vikundi vya ngoma za kitamaduni!!




Vikundi mbalimbali vya ngoma za kitamaduni vikitumbuiza wakati wa uzinduzi wa maadhimisho rasmi ya siku ya malaria ambapo kilele chake ni hapo kesho tarehe 25 April 2009.

Umati siku ya Uzinduzi Malaria.



Pichani ni umati wa wananchi wa Mtwara waliojitokeza siku ya uzinduzi wa Malaria Day.

Malaria Day Mtwara!

Moja ya mabanda katika kuadhimisha siku ya malaria duniani.
Hii ni idara ya Damu salama.

Mabanda ya idara za afya yote yaliwepo.

Banda la Tiba nalo liliwepo.



Wadau wengine wanaojihusisha kwa namna moja ama nyingine katika mapambano dhidi ya malaria wapo katika kuadhimisha siku hii ya malaria ambapo kilele chake ni tarehe 25 april 2009 Mheshimiwa waziri Mkuu akiwa mgani rasmi. Habari za kufurahisha ni kwamba Lady JD na Ivyone Chakachaka tayari yupo mjini Mtwara Leo.