Friday, January 23, 2009
Hii ni Imani au Baraka?
Nimebahatika kuona pindi niwapo katika mizunguko yango ya kila siku vijijini kwa gari na kushuhudia nyuma baada ya kupita kwa baadhi ya wanavijiji huchukua wanao wadogo na kwenda kuwakanyagisha zilipoacha/pita alama za matairi ya gari. Nimeshindwa kujua bado mpaka sasa ni nini maana yake!?
Wewe una ufahamu wowote juu ya hili?
Mzani!!
Nilibahatika siku moja kukuta Nurse akisisitiza kwa akina mama kuja na kikalio kama kionekanacho pichani kwa ajili ya kupimia uzito watoto. Nurse huyo aliwaomba akina mama kushonesha kila mtu chake kuepuka kuambukizana magonjwa ya ngozi kati ya mtoto mmoja kwenda kwa mwingine. Kwa kweli nilifurahishwa na hilo hope pia wewe utasambaza elimu hii kwa jamii iliyokuzunguka.
Hali halisi
Subscribe to:
Posts (Atom)