Sunday, February 8, 2009

Duniani!

Maisha hayafanani.

Hili ndilo Tanuli la matofali...

Katika maisha yangu kwa mara ya kwanza Tanuli kama hilo pichani nililifahamia mkoani Mbeya enzi za Sekondari.

Msongamano...

We unadhani walikuwa wanafanya nini hapo?

Kutoka maktaba!


Mshangao...

Watoto hawa niliwakuta wakilishangaa greda wakati wa ujenzi wa barabara, miongoni mwao labda mmoja wao anayo-vision ya kuja kuwa mkandarasi hatuwezi fahamu kwa haraka.

Mnazi mmoja ya Lindi

Upende niliopo mimi ni kutokea wilaya ya Masasi (Mtwara).
Ambapo kulia kwangu ni kuelekea Mtwara na kushoto Lindi.
Na hiki ni kituo cha mizani mnazi mmoja hapo hapo.


Water tank in Rural...

Moja ya aina ya matenki ya maji yaliyojengwa vijijini na miradi mbali mbali ya kimaendeleo.

Petrol station...

Mambo kwa vidumu tu.

Mchakato wa usafiri unaendelea...

Usivae suti utashiba na kuoga vumbi kama si matope kipindi cha mvua.

Taswira!

Ni moja ya biashara zinazowepa ugali vijana wa vijijini.

Mikoko @Mikindani

Mazalio ya samaki kwenye mikoko iliyopo pembezoni kabisa mwa ufukwe wa Mikindani (Mtwara), kwa waliosoma historia vizuri wataijua Mikindani.

Nazi nazi nazi!!