Sunday, January 25, 2009

Anaconda

Aisee huyu ndie Anaconda.

Daraja mbao


Sunset


Moja kati ya aina ya picha ninazozipenda sana, hasa kwa kupamba ndani ya nyumba huleta nakshi nzuri sana.

Sehemu za kufurahia maisha

Moja ya resort almaarufu Sunrise Beach Resort, kwa maraha na beach safi hapa ndio mahala pake. Tembelea Kigamboni Dar es Salaam almaarufu eneo linaitwa mjimwema.

Twende Kazi!


Ufahamu kuhusu ugonjwa wa TB

Ili mtu aweze kuugua TB ni lazima awe na mgonjwa aliemuambikiza TB, na yeye awe na upungufu wa kinga mwilini. Upungufu wa kinga mwilini unaweza kusababishwa na maradhi mbalimbali yakiwemo:
Utapiamlo, Kisukari, Surua, UKIMWI na mengineyo.
Pia kinga ya mwili inaweza kupungua ukitumia dawa za kutibu saratani au za kushusha kinga ya mwilini.

Dalili za TB.
Kukohoa mfululizo kwa muda wa wiki mbili (2) au zaidi, na kutoa makohozi safi yaliyochanganyika na damu.
Maumivu ya kifua.
Kutokuwa na hamu ya kula.
Kukonda na kupungua uzito wa mwili na kunakoendelea.
Mwili kunyong’onyea na kuhisi uchovu.
Homa mfululizo.

Nazi na mti wake

Kwa watu wa mikoa ya pwani nazi huwa ndio kiungo mbadala ya mafuta ya kupikia yanayolalamikiwa na wengi kiafya kuwasumbua. Wewe unasemaje kuhusiana na nazi?

Stone town

Moja ya mitaa ya stone town ndani ya Zanzibar mji mkongwe.