Thursday, February 5, 2009

Kazi ya watoto ukutani...!!


Mkaa sokoni

Nunua na kiroba chake au unabadilishana na kiroba kingine, ndio biashara.

Tandahimba saaafi kabisa.



Pichani ni majengo mapya ya Hospitali ya wilaya ya Tandahimba (Mtwara) yakiwa katika hatua ya mwisho kabisa. Kazi kwao wananchi siku za usoni kuyatunza.


Pata hii kwenye maelezo...

Pichani sikuweza kuwapata wote ila ni baadhi ya vijana wakiwa chini ya mti majira ya saa tatu asubuhi. Hii nimeishuhudia sana vijijini mkoani Mtwara kwa vijana kulundikana vijiweni wakati wa kazi. Sio kwamba ardhi haipo ya kujishughulisha! Hapana jibu ni ipo, hiyo ndio hali kalisi.

Niwapo vijijini hii ndio pasi


Ukiwa kijijini huwezi kuikwepa hii, ingawa hata mijini wapo wanaozitumia mapaka leo.

Unakumbuka nini pichani?


Msumeno wa magogo huo...

Hiyo ndio sampo ya misumeno itumikayo kukata magogo makubwa.
Hushikwa na watu wawili wakati wa kazi.

Jua linapokuwa kazi...