Wednesday, January 28, 2009

Comment!!!


Kutoka maktaba

Jumba la maajabu Zanzibar! Pembezoni kabisa mwa Forodhani ya zamani, kwa sasa forodhani ipo katika mchakato wa mwisho mwisho kakamilika pawe pa kisasa zaidi.

Mawaziri wa baadae hao!

Wakati mtoto wa kijijini kushika muhogo na kuutafuna mbichi mbichi ni kawaida, wa mjini analilia nya kwenye pakti... Maisha hayafanani kabisa.

Mambo ya patastories hayo!


Kukuz


Hii kali...

Dada hapo yupo bize kuisaini kijistika ndogo kwa ajili ya kumpatia mteja anaekuja kuacha simu yake kwaa ajili ya kuichaji, hii yote kuepukana na mafisadi wa simu wataodai kuwa waliacha za kwao zikichajiwa. Mambo ya kijijini hayo, tembea uone.

Stand ya Mabasi Masasi (Mtwara)


Bajaji, pikipiki mabasi, daladala mabasi makubwa ili mradi kila kimojawapo kina lake jambo.

SACCOS


Usiwe kama kobe!


Taswira!


PPF tower ya mchwa!

Ghorofa hili limejengwa na mchwa, wadudu hawa wanaushirikiano wa hali ya juu. Siku moja nilibahatika kupita na kuingia nyumba moja kijini na kukuta pamebomolewa kitu mfano wa huo pichani. Nikauliza wakasema ni mchwa hao, na kubomoa tu hakusaidiii maana wanajenga tena, watalamu husema mpaka apatikane malkia wao mchwa ndio wanahama na wenyewe kazi ambayo sio nyepesi kama unavyoifikiria.

Friji la kutumia gesi.

Haya ni mafriji yanayotumika katika mazahanati mengi vijijini kuhifadhia dawa, yanatumia nishati ya gesi hivyo kufanya hata pasipo na umeme kuwepo na huduma hii muhimu.

Fahari ya Mtwara

Hii ndio fahari ya Mtwara, kwa waliowahifika si kitu kigeni. Maendeleo siku hizi ni kwenye chupa kubwa kama makampuni mengine makubwa yanayojulikana.

Mbegu dukani...


Korosho hizooo!


Dawa mseto ya malaria!

Wale wavivu na waoga wa kumeza dawa hii itakuwa kama adhabu kwao.
Ni mseto tuu mpaka unamaliza dozi.

Kokoto nyeupe!


Umewahi kukutana na kokoto za rangi hii?