Tuesday, January 27, 2009

Wanafunzi!!

Kutokana na shule wasomayo ina kaumbali ka kutosha mpaka maeneo wanayoishi, baiskeli huwa ndio usafiri wa haraka kwa wanafunzi hawa.

Linakukumbusha nini hili Trekta?


Video show...


Uwapo kijijini na ukashuhudia kasha la Video kaseti likining'inia kwa mtindo huo linamaanisha kuwa nido picha itayoonyeshwa kenye kaukumbi husika kwa kiingilio cha kati ya shilingi hamsini na mia. Na kikubwa zaidi picha hizo kuwazanakuwa na mtu anaetafsiri iwe ya kihindi nk
Nakushauri siku moja ukiwa kijijini ingia sehemu kama hizo usikie yanayozungummzwa na kutafsiriwa ufe mbavu.

Matafali ya kuchoma!

Uzoefu unaonyesha kwa vijijini, wenye kauwezo uwezo huwa wanajenga nyumba zao kwa matofali ya aina hii. Na mwenye uwezo mkubwa zaidi hujenga kwa ya cement.

Nyigu mlangoni

Inakuwaje upo kijijini fulani na unaambiwa hapo chini ya mlango ndio inapopatikana network ya mtandao fulani wa simu ya mkononi, uoga au ujasiri kipi kitangulie?

Kisima chakavu


Mahindi

Wanaposema mahindi yameungua huwa vivyo pichani, hii inatokana na kuchelewa kwa mvua. Waswahili husema hali kama hiyo ikitokea ni imekula kwako.

Mishikaki!

Mishikaki inayopendeza baada ya kutiwa viungo kabla ya kuchomwa, huwezi kula mmoja lazima utaagiza wa pili na kuendelea...

Moja ya Hospitali kongwe!




Moja ya hospitali za zamani nchini Tanzania, hospitali hii ni ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara. Kwa waliofika Masasi kwa namna moja ama nyingine wana/watakuwa wanaijua.


Waijua karanga shambani?

Huu/hii ndio karanga mimea yake.

Kiti cha mgonjwa!

Kiti hiki nimekifuma katika moja ya zahaniti jina kapuni.

Lami na ukandarasi...


Katika pita pita zangu nilibahatika kulifuma/kuyafuma magari hayo moja likiwa la kupika lami lingine la umwagaji wa lami hiyo. Wapi yanaenda sikuwa na ufahamu.

Biashara matangazo


Karibu tujichane...

Nilibahatika kukutana na huyo mtoto ni muongeaji sana na aliniambia ana meno makali kwa kumenya na kuushughulikia muwa.

Dish na Kutu

Inachekesha ila ni kweli, ilitokea jamaa mmoja dish lake lilipata kutu zaidi ya ulionalo, na akaamua kulipaka rangi. Kilichofuata hakupata channel hata moja tena. Je, yawezekana rangi inayowepo awali kabla ya kutu ina umuhimu wake?

Shule aliyosoma Rais mstaafu awamu ya tatu


Chidya Boys, ipo Mkoani Mtwara wilaya ya masasi. Pichani ni baadhi ya majengo ya shule hiyo.

Kodisha upendayo...

Sio Tanga tu biashara hii wala Morogoro, Mtwara nako baadhi ya wilaya ipo.

Ajali za pikipiki

Ajali za pikipiki

Kumekuwa na tabia ya baadhi ya wilaya nazitolea mfano nilizopita mimi mfano Wilaya ya Masasi, Nanyumbu na hata Newala mkoani Mtwara sijui mikoa mingine. Pikipiki zimekuwa zikiendeshwa kwa speed kubwa sana na kuwa kero kubwa kwa wastaarabu, leo tarehe 26.1.2009 kumetokea ajali tatu (3) tofauti kwa wakati tofauti na kupoteza maisha ya aidha waenda kwa miguu ama aliyepakia ama wote pamoja na dereva mwenyewe.

Ajali za pikipiki zinamajeraha mabaya sana hilo sote tunatambua lakini je, hawa vijana wanaozikimbiza pikipiki hizi tuwaitaje? Makatili, viburi au jeuri ndio inawafanya wawe vichwa ngumu. Tetesi zinasema wengi wa vijana hao ambao huendesha pikipiki hizo almaarufu kwa jina la SANLG inasemekana walikuwa wakiuza maji kwenye madumu hapo awali, je kuhamia kwenye biashara ya kupakia abiria imekuwa sababu ya kujihesabu na kuleta ujuzi kwenye mambo ya hatari ya kwenda mwendo wa kasi kupita kiasi?

Hivi sasa moja ya hatua ambayo nimeiona ni kuwekwa matuta kwa baadhi ya barabara lakini bado kwenye njia zilizobakia hali ni vilevile. Kwa kweli ni tabia ambayo si nzuri na haifai kuigwa. Kwa waliobahatika kufika maeneo husika watakubaliana nami hali hiyo ilivyokuwa sugu. Nakutakia siku njema.

Wako Mdau,
John.

Aina ya pikipiki husika

Hata watoto wamo!

Ndani ya kijiji kimoja nilipendezwa na hawa watoto.

Ambulance


Kibanda

Kibanda hiki sio tu kama ni cha mapumziko... bali...





Ni Bakery kama zilivyo zingine kwa kuoka mikate, sijafahamu wanafanyaje ila habari ndio hiyo. Mikate kwa kijijini hapo huokwa hapo kitaalamu.