Saturday, February 7, 2009

Sare za shule.

Zenye ukijani ukijani ni kwa chekechea, na zingine bluu na nyeupe ni zile zile tulizovaa mimi na wewe mwenzangu tuliesoma St. Abdalah!

Kumbikumbi Weusi!

Wakiviziwa toka shimoni.
Baada ya kudakwa kabla hawajaruka.

Baada ya kupikwa.
Mimi binafsi ndio mara ya kwanza nawaona wadudu hawa na cha kushangaza nimeambiwa wanaliwa. Kumbikumbi niwajuao mie sio type hii ya leo.
Tembea uone.



Cheka kiafya!


Kutoka Maktaba!!

Sio vita, ni sherehe za kimila ambazo hufanyika kila mwaka huku visiwani (Zanzibar).
Pichani moja ya walioenda kushuhudia aliamua kujitosa kukamilisha shughuli hiyo.

Wakati wa kupeana kipondo huwa wanatumia migomba na si mmea mwingie wowote kuepusha majeruhi wakati wa sherehe kama hizo almaarufu kama "Mwaka koga"

Vijana wakionyeshana maujuzi wakati wa kuchapana na silaha Mgomba.

Hapa ni mchakamchaka kabla ya shughuli yenyewe kuanza, huwa wanaimba nyimbo ambazo hata ukizi-edit bado hazifai katika jamii yetu ya Mtanzania mstaarabu kama wewe.

Wakina mama nao huwa hawakubali kuachwa nyuma.
Mwaka huu sitobahatika kuwepo eneo husika nikupatie vionjo.


Alini-time kiukweli kweli hapa!!

Hata habari sikuwa nayo wakati ikiviziwa picha hii.

Taswira!!


Hii kali...!!

Hali kama hii inapotokea hakuna jinsi zaidi ya kushusha mzigo wote chini ili kazi ya kulinasua lori ifanyime. Upande wapili wa lori hili kuna magunia ya korosho yameshushwa kutokana na uzito.

Melbourne hiyo jamani (Australia)



Duniani huko jamani, mipango miji nk ipi juu sana.


Umeme jua! umeme jua!

Hapo pichani ni pembezoni wa duka ambapo mhusika anajipatia umeme wake kiulaiiini huku batter zikichajiwa kwa matumizi ya baadae (Usiku). Mambo ya vijijini hayo.

Ukandarasi!!

Trekta aina ya Valment halipo nyuma katika ujenzi wa barabara, usisahau shambani nako linavuma. Hii ndio hali halisi huku "up-countries" tembea uone.

Chambua picha hizi...

Kwa wabongo unaweza sikia eti hayo maganda ya Madafu deal.

Kuni imezoeleka kuwa deal, ingawa inachangia uharibifu wa mazingira.

Mawe haya yaliyobomolewa toka nyumba za kuishi watu nayo ni deal kwa wengine.

Wewe una lepi?


Eneo nililojidai nalo enzi zetu...

Kwa mkazi wa Dar na kwingineko waliowahi kupasikia Mabibo hostel watakuwa wanajua nazungumzia nini. Ni moja ya Hostel za Chuo Kikuu Dar es Salaam, waliopita hapo hakika watakubaliana na mimi kuwa pana mazingira yanayovutia.

Tudumishe majengo yetu!

Pamoja ya kwamba maghala haya ni ya siku nyingi me napendenzwa nayo kwa jinsi yanavyoboreshwa na kutunzwa. Yapo Mkoani Lindi sehemu inaitwa Mtama.

Gogo njiani!!

Pamoja na kukuta mti huu umeanguka njiani, shukrani kwa wale waliochukua hatua za haraka kusababisha njia iendelee kutumika, vinginevyo hali ingekuwa mbaya zaidi kwa wenye magari.
Pamoja na hayo wadau niliwaona wamejipatia mbao bwerere toka gogo hilo.