Monday, September 7, 2009

Sijui nikiite kimwagilia majani?


Niliifuma Mafinga hii style ya kumwagilia, chupa ya maji ya plastiki iliyochomekwa pamoja na mpira then matundu yaliyopo kwenye chupa yakipenyesha maji na kumwagilia nyasi.

Sambusa za mchele???

Tumezoea kuona Samosa za nyama ndani ama viazi, lakini hizi pichani ndani zina mchele uliopikwa sio mbichi. Kweli tembea uone.

Kweli tembea uone...

Staajabu uyaonayo pichani...
Hilo ulionalo ni mfano sambamba na bomba la maji, ukikanyaga huo mti dumu la maji linainama na maji yanamiminika.
Hivyo hapo ni vitundu vya kupitishia maji unapohitaji kunawa nk.

Uboreshaji Daftari la wapiga kura vijijini!


Uboreshaji wa daftari la wapigakura, technolojia ikiwezesha zoezi kwa kutumia nishati ya jua.

Umeiona Heater hiyo ya kienyeji?


Utaalamu na ubunifu upo wa aina mbalimbali, picha hii nimeipiga nikiwa Mafinga mkoani Iringa kunako baribi kweli kweli.