
Wednesday, January 28, 2009
PPF tower ya mchwa!
Ghorofa hili limejengwa na mchwa, wadudu hawa wanaushirikiano wa hali ya juu. Siku moja nilibahatika kupita na kuingia nyumba moja kijini na kukuta pamebomolewa kitu mfano wa huo pichani. Nikauliza wakasema ni mchwa hao, na kubomoa tu hakusaidiii maana wanajenga tena, watalamu husema mpaka apatikane malkia wao mchwa ndio wanahama na wenyewe kazi ambayo sio nyepesi kama unavyoifikiria.Tuesday, January 27, 2009
Video show...

Uwapo kijijini na ukashuhudia kasha la Video kaseti likining'inia kwa mtindo huo linamaanisha kuwa nido picha itayoonyeshwa kenye kaukumbi husika kwa kiingilio cha kati ya shilingi hamsini na mia. Na kikubwa zaidi picha hizo kuwazanakuwa na mtu anaetafsiri iwe ya kihindi nk Nakushauri siku moja ukiwa kijijini ingia sehemu kama hizo usikie yanayozungummzwa na kutafsiriwa ufe mbavu.
Subscribe to:
Posts (Atom)












