Tuesday, February 24, 2009

Kutoka ushauri na maoni mbali mbali

Nianze kwa kuwashukuru mnao nipatia muda wenu na kupita katika blog yangu kuperuzi hili na lile. Lingine lililoniofanya niandike ujumbe huu ni kwamba, baadhi ya wadau kwa namna moja ama nyingine wameomba kuwepo pia picha zinazogusa/zungumzia mazingira na mila pamoja na desturi za huko vijijini nipitako kila kukicha. Jibu nililokuwa nalo la haraka haraka la kueleweka ni kwamba:
Mimi binafsi ni mfanyakazi wa NGO fulani hivyo kupata picha za mila na desturi nk inakuwa ngumu kwa sababu muda wangu mwingi nakuwa bize na kazi inayonipatia ugali.
Pili, sitoweza tumia muda wa kazi kwa kufanya mambo yangu binafsi kwani kazi ni kitu ninachokiheshimu kuliko ugali ninaokula.
Tatu, picha unazozipata (vionjo) unavyovipata ni matokea ya yale ambayo kwa namna moja ama nyingingine nimekuwa nikikutana nayo wakati nikiwa eneo husika, hivyo basi niwaombe radhi kama kuna machache nitakuwa nakunyima kutoka pande za vijijini.
Pamoja na hayo nakutakia siku njema yenye baraka.
Pia nashukuru kama umenielewa maneno yangu.
Wako Mdau.

1 comment:

  1. Tunakuaminia mkurugenz, endeleza libeneke mwana.
    leta vitu utakavyokuwa unapata tuweze kuona ishu zinavyoendelea huko kusini

    Merci beacoup!!

    ReplyDelete

Be good.