Tuesday, March 31, 2009

Kuuliza si ujinga...!!

Naomba kuuliza, Hili ni tunda gani eti?

Una utamaduni wa kula matunda?


Ni swali la kizushi lakini lina umuhimu sana, tathmini.
Mwili haujengwa kwa matofali.

Yaliyojiri...

Hapa baada ya kupata chai mgonjwa huyu wa akili akipayuka yaliyokitoka katika kinywa chake.

Mgonjwa huyu wa akili nilimkuta akipata chai mgahawani kama pichani inavyoonekana.

Hapa baada ya kumaliza chai akisokota bangi tayari kuipuliza, kabla hajaanza kuisokota alikuwa akipayuka ile mbaya bila kujua ni nani saha anayempayukia toka kinywani mwake.
Huku akisisitiza siogopi mtu nalipuliza hapa hapa nje.
Utajiuliza hizo bangi anazipatia wapi na nani anampatia mimi na wewe sote hatuna majibu.

Thursday, March 26, 2009

Harakati za kupambana na Maleria pichani.

Watendaji kadhaa wa vijiji wakishiriki mafunzo.

Uji barabarani...

Umewahi kusikia/kuona uji nao ukitembezwa barabarani kama inavyouzwa kahawa?
Mimi niliifuma wilayani Masasi (Mtwara). Kibaya zaidi wanaouza wenyewe wanakuja mpaka bar, je bar utamuuzia nani na watu tayari wana-alcohol kadhaa kichwani???
Kweli wanasema tembea uone.

Wanapendeza na sare mpya!

Monday, March 23, 2009

News!

Baada ya muda mrefu camera ya blogspot kuna na matatizo yaliyokuwa nje ya uwezo wangu, hatimaye imepona na ipo njiani kuendeleza libeneke. Soon wadau wa blog mtapata picha quality.
Nikutakie siku njema.

Pole Paradise and Ocenic Bay!

Blog ya patastories inatoa masikitiko yake kwa yaliyotokea Paradise Hotel na Ocenic Bay.
Kwakweli hasara iliyotokea pale ni kuubwa saana, kwa wale wanaozijua vizuri hotel zile kama mimi ama kulala hata one night watajua namaanisha nini. Nashindwa hata kuzungumzia kwa hali niliyoiona kupitia blog ya michuzi. Nimesikitika sana as if am one of the owner. Nawapa pole zangu nyingi bila kipimo waliohusika na hasara hiyo kwa namna moja ama nyingine.

Friday, March 20, 2009

Ujumbe huo...!

Wanafunzi waliofaidika kwa misaada toka mashirika ya kidini.

Wakionyesha nyuso za furaha wanafunzi hao wa shule ya msingi wakionyesha moja ya zawadi walizopatiwa.

Jumuiya za Dini zinavyofanikisha maendeleo ya wananchi


Wananchi kwa pamoja wakijumuisha nguvu katika maendeleo.

Jamii ikiwana ushiriki katika kutimiza malengo.

Moja ya jamii zilizofaidika na jumuiya za kidini.

Thursday, March 19, 2009

Ngumi asubuhi asubuhi!


Vijana hawa walikuwa wakionyeshana ubabe, sababu ya ugomvi wao ni kudaiana hela. Mimi nilikuwa mpita njia tu majira hayo ya saa mbili asubuhi.

Enzi zetu ilikuwa vi-soda...


Kijijini watoto wa shule za msingi wao hutumia vipande vya miti kuhesabu, enzi za mwa.a.a.limu tulitumia visoda. Siku hizi watoto wa shule za dot.com wanavifaa maalumu. Maisha yanaenda yakibadilika kila kukicha.

Baghdad ya Mtwara


Sio ya kule Iraq... No. Hapo ni kijijini Chiungutwa (Masasi District) -Mtwara

Tuesday, March 17, 2009

Kuku mgeni...???

Msala kwenye kona!

Basi hili lipo kwenye kona kiasi kwamba kama hatua za tahadhari hazikuchukuliwa kunaweza kutokea maafa.

Aajali kwenye nguzo

Hapo ni kwamba gari liliivamia nguzo hiyo na bahati nzuri nguzo husika haikuwa na nyaya za umeme. Sijui hali ya gari ilikuwaje na driver. Picha kwa hisani ya Edga.