Ni habari ya kweli sio hadithi: Ilitokea siku moja wanakijiji walimpeleka mgonjwa wao zahanati ya kijiji. Walipofika zahanati kwa sababu mgonjwa wao alikuwa anaumwa sana wakaandikiwa rufaa ya kwenda katika hospitali ya rufaa (wilayani). Cha kuchekesha na kusikitisha baadhi ya wauguzi (wanakijiji) wa mgonjwa huyo wakamletea mganga wa zahanati hiyo jogoo ili awaahirishie safari ya kwenda hospitali ya wilaya. Yule mganga alishikwa na butwaa na kuwashangaa sana bila majibu. Mganga msimamo wake ulibakia pale pale, alibaki kuwauliza kuthamini utu na huyo jogoo je walifikiria mara mbili au?
Hivi ni vijimambo vya vijijini.
Hivi ni vijimambo vya vijijini.
No comments:
Post a Comment
Be good.