Tuesday, January 27, 2009

Ajali za pikipiki

Ajali za pikipiki

Kumekuwa na tabia ya baadhi ya wilaya nazitolea mfano nilizopita mimi mfano Wilaya ya Masasi, Nanyumbu na hata Newala mkoani Mtwara sijui mikoa mingine. Pikipiki zimekuwa zikiendeshwa kwa speed kubwa sana na kuwa kero kubwa kwa wastaarabu, leo tarehe 26.1.2009 kumetokea ajali tatu (3) tofauti kwa wakati tofauti na kupoteza maisha ya aidha waenda kwa miguu ama aliyepakia ama wote pamoja na dereva mwenyewe.

Ajali za pikipiki zinamajeraha mabaya sana hilo sote tunatambua lakini je, hawa vijana wanaozikimbiza pikipiki hizi tuwaitaje? Makatili, viburi au jeuri ndio inawafanya wawe vichwa ngumu. Tetesi zinasema wengi wa vijana hao ambao huendesha pikipiki hizo almaarufu kwa jina la SANLG inasemekana walikuwa wakiuza maji kwenye madumu hapo awali, je kuhamia kwenye biashara ya kupakia abiria imekuwa sababu ya kujihesabu na kuleta ujuzi kwenye mambo ya hatari ya kwenda mwendo wa kasi kupita kiasi?

Hivi sasa moja ya hatua ambayo nimeiona ni kuwekwa matuta kwa baadhi ya barabara lakini bado kwenye njia zilizobakia hali ni vilevile. Kwa kweli ni tabia ambayo si nzuri na haifai kuigwa. Kwa waliobahatika kufika maeneo husika watakubaliana nami hali hiyo ilivyokuwa sugu. Nakutakia siku njema.

Wako Mdau,
John.

Aina ya pikipiki husika

Hata watoto wamo!

Ndani ya kijiji kimoja nilipendezwa na hawa watoto.

Ambulance


Kibanda

Kibanda hiki sio tu kama ni cha mapumziko... bali...





Ni Bakery kama zilivyo zingine kwa kuoka mikate, sijafahamu wanafanyaje ila habari ndio hiyo. Mikate kwa kijijini hapo huokwa hapo kitaalamu.

Monday, January 26, 2009

Ukweli... Tathmini...


Kutoka maktaba

Picha hii niliipiga Zanzibar, sio mbaya tukijikumbusha mambo ya forodhani pembezoni kabisa mwa bahari ya hindi.

Kipimo...

Hata kama ungeambiwa tikiti moja lina sumu ungelitambua?

Speed Limit


Jiji la Mwanza pichani


Tangazo


Mkorosho!!

Moja ya mikorosho inayotarajiwa siku za usoni. Kwa kawaida unapokuwa unazaa majani majani yote chini hufyekwa kuepusha wadudu waharibifu. Zao maarufu mikoa ya Lindi na Mtwara kwa kusini.

Nakshi nzuri nyumbani

Mimi binafsi ni mpenzi sana wa sebule nzuri zenye kupendeza, rangi zisizopishana kupitiliza nk Mfano huo pichani ni dondoo tamu ukapata ka-kuiga kidogo na wewe.

Nani zaidi...


Biashara ya mbao mpakani!

Pichani ni mbao zinazovushwa toka Msumbiji kwa mitumbwi midogo tayari kwa biashara.

Njia panda...


Kwa wakazi wa maeneo ya Ndanda (mtwara) si pageni kwo, hapa ni njia panda kwenda chanzo cha maji almaarufu Ndanda Spring Water. Karibu siku moja utembelee.