Tuesday, January 27, 2009

Ajali za pikipiki

Ajali za pikipiki

Kumekuwa na tabia ya baadhi ya wilaya nazitolea mfano nilizopita mimi mfano Wilaya ya Masasi, Nanyumbu na hata Newala mkoani Mtwara sijui mikoa mingine. Pikipiki zimekuwa zikiendeshwa kwa speed kubwa sana na kuwa kero kubwa kwa wastaarabu, leo tarehe 26.1.2009 kumetokea ajali tatu (3) tofauti kwa wakati tofauti na kupoteza maisha ya aidha waenda kwa miguu ama aliyepakia ama wote pamoja na dereva mwenyewe.

Ajali za pikipiki zinamajeraha mabaya sana hilo sote tunatambua lakini je, hawa vijana wanaozikimbiza pikipiki hizi tuwaitaje? Makatili, viburi au jeuri ndio inawafanya wawe vichwa ngumu. Tetesi zinasema wengi wa vijana hao ambao huendesha pikipiki hizo almaarufu kwa jina la SANLG inasemekana walikuwa wakiuza maji kwenye madumu hapo awali, je kuhamia kwenye biashara ya kupakia abiria imekuwa sababu ya kujihesabu na kuleta ujuzi kwenye mambo ya hatari ya kwenda mwendo wa kasi kupita kiasi?

Hivi sasa moja ya hatua ambayo nimeiona ni kuwekwa matuta kwa baadhi ya barabara lakini bado kwenye njia zilizobakia hali ni vilevile. Kwa kweli ni tabia ambayo si nzuri na haifai kuigwa. Kwa waliobahatika kufika maeneo husika watakubaliana nami hali hiyo ilivyokuwa sugu. Nakutakia siku njema.

Wako Mdau,
John.

Aina ya pikipiki husika

No comments:

Post a Comment

Be good.