
Friday, January 30, 2009
Ukweli kuhusu Prison Break
Prison BreakUkweli kuhusu Prison Break, imezoeleka masikioni na machoni mwa wengi kuona mitaani Prison Break inapatikana mpaka season eight (8). Hii nathibitisha wazi kuwa Prison Break kihalisia haijafika season eight (8). Hizi mnazoziona mitani ni Episodes tu toka season halali season four (4).
Kwa wanaofuatilia kwa makini watajua ninamaanisha nini. Ukweli ni kwamba kibiashara tu ili kupata pesa wadau Fulani fulani ili wasilale njaa ndio wameamua kuikata kata vipande “episodes” hizo na kuzigawanya katika mafungu wayajuayo wenyewe na kuyaita “season Fulani mpaka Fulani. Ukweli unabaki pale pale kuwa wananchi wamekuwa wakinunua season moja mara nne zaidi bila wao kujua. Ila kutokana na utamu wa sinema yenyewe then watu kwao ni sawa tu bora kuona.
Ilikuwa ni katika kupeana dodoso tu habari ndio hiyo ipo nje nje.
Thursday, January 29, 2009
Ukisikia mkonge ndio huu!!!
Kama inavyoonekana pichani, mkonge wa moja ya gari za kazi Land Cruiser ukiwa umechomewa kwa lengo kuubwa la kupambana na vibaka. Inasemekana gari kama hiyo pindi (Mfano) ipatapo ajali wale wapenda kung'oa vifaa hukimbilia huo mkonge. Habari zinasema kwamba unagharama kuubwa sana ndio sababu ya vibaka kuwinda ulaji huo wanaojua/fahamu magari wanaelewa hilo.Nauli!
Inasemekana kuwa kwa baadhi ya magari almaarufu makenta ama malori yabebayo abiria yanayofanya safari zake kwenda Tunduru kupitia njia ya Mtwara wanawake ndio hulipa nauli kubwa, hili nikauliza na kujibiwa kuwa baadhi ya makenta/malori hayo ni vimeo (Mabovu) hivyo linapohitaji msaada wa kulisumkuma liwake wanaume ndio wanashughulika. Swali je kwa mwanaume akitaka kulipa nauli kubwa kidogo na yeye atakubaliwa?
Wednesday, January 28, 2009
Subscribe to:
Posts (Atom)












