Sunday, February 1, 2009
Saturday, January 31, 2009
Teknolojia...
Teknolojia moja inapoipiku ingine huua kwa namna moja ama soko wa iliyopita, pichani ni kifaa chenye uwezo kama flash disk kenye uwezo wa kuhifadhi na kusikiliza mziki uwapo garini. Ni teknolojia nzuri sikata, hasa kwa barabara za vijijini ambapo CD kwenye kashkash za rafu road inakata kuimba. Wanasema Mchina huyo bwana.Friday, January 30, 2009
Cheka Kiafya!!
Kuna sehemu moja Mkoani Mtwara inaitwa Nakapanya na ingine inaitwa Nanguruwe, hii ni kweli na ucheke kiafya tu sio sana. Kuna dada mmoja wakati mahojiano yakiendelea kuhusu maisha yake nk, nk, ilifika kipindi katika maelezo yake ilikuwa hivi:...mimi niliolewa Nakapanya nikaachika nikaenda kuishi Nanguruwe...
Yaani akimaanisha aliwahi ishi maisha ya ndoa Nakapanya na baadae akaenda kuishi Nanguruwe.
Ni story ya kweli si ya kutunga.
Kiafya tafadhali!
Hali halisi kipindi cha mvua...
Watoto hawa nimewakuta wakicheza kwenye maji yaliyotuama ya mvua. Yawezekana shida ya maji vijijini hufanya mpaka hali kama hii ikitokea watoto hawa husherekea. Na wazazi wao sio kwamba walikuwa mbali na watoto hao? Hapana.
Huyu ndie nisema kama kwenye swimming pool basi ndio yupo deep.Vijimamboz hivyo na patastories.
Subscribe to:
Posts (Atom)



















