Sunday, February 1, 2009

Sokoni mashalah!

Kaka ame-display picha zake sokoni za yeye na wateja wake. Ni unique style.

African Art...


Nakshi nzuri kwa sebule yako.
Waswahili wanasema kizuri gharama.

Sio kibaba... ni loki ya bomba la maji.

Kwa wale wauza au wanunua maji ya bomba hili si geni kabisa kwao. Kwa mtazamo wa kwanza unaweza sema ni kibaba kitumikacho kuhifadhia sarafu za pesa.

Dawa!!

Moja ya dawa ta aina yake ambayo kabeji zimelowekwa kwa ajili ya kituo kimoja kinachohudumia watu wanaoishi na VVU.

Greda bar...

Nalo limeenda kupata supu na mtori.

Umeiona hii?
















Saturday, January 31, 2009

Kwa wapenda Magari...

Link ifuatayo chini inaweza kukupa idea fulani kuhusu gari yako...

Fm Academia ndani ya Mtwara

Wazee wa Ngwasuma wakianza shughuli nzima.
Hizi zote ni mbwembwe kuwakonga wadau ukumbini.

Palikuwa hapatoshi.


Wadau na wapenzi wa Ngwasuma hawakuwa nyuma.

Ni full shangwe na Ngwasuma.





Teknolojia...

Teknolojia moja inapoipiku ingine huua kwa namna moja ama soko wa iliyopita, pichani ni kifaa chenye uwezo kama flash disk kenye uwezo wa kuhifadhi na kusikiliza mziki uwapo garini. Ni teknolojia nzuri sikata, hasa kwa barabara za vijijini ambapo CD kwenye kashkash za rafu road inakata kuimba. Wanasema Mchina huyo bwana.

Kijiweni...

Kwenye majengo wanapopangisha wanalipa kodi, je hapa napo vivyo hivyo? Swali.

Friday, January 30, 2009

Na hili je?

Unapoletewa maji kama haya je mara zote unakuwa na uhakika yanapotoka?
Au tunaangalia shida ilivyotubana tu...?

Cheka Kiafya!!

Add ImageKuna sehemu moja Mkoani Mtwara inaitwa Nakapanya na ingine inaitwa Nanguruwe, hii ni kweli na ucheke kiafya tu sio sana. Kuna dada mmoja wakati mahojiano yakiendelea kuhusu maisha yake nk, nk, ilifika kipindi katika maelezo yake ilikuwa hivi:
...mimi niliolewa Nakapanya nikaachika nikaenda kuishi Nanguruwe...
Yaani akimaanisha aliwahi ishi maisha ya ndoa Nakapanya na baadae akaenda kuishi Nanguruwe.
Ni story ya kweli si ya kutunga.
Kiafya tafadhali!

Ni mapambo tu sio wa ukweli.

Anaweza kuwa kivutio kama ni nyumbani kwako, garden nk nk.



Usafiri wetu kijijini ndio huooo!!

Hali ndio kama hivyo pichani, ukikosa Land Rover almaarufu Muhogo basi utapanda Kenta ama Lori. Ya mjini mjini na kijijini kijijini tu.

Hali halisi kipindi cha mvua...

Watoto hawa nimewakuta wakicheza kwenye maji yaliyotuama ya mvua. Yawezekana shida ya maji vijijini hufanya mpaka hali kama hii ikitokea watoto hawa husherekea. Na wazazi wao sio kwamba walikuwa mbali na watoto hao? Hapana.
Huyu ndie nisema kama kwenye swimming pool basi ndio yupo deep.
Vijimamboz hivyo na patastories.