
Wednesday, February 11, 2009
Tuesday, February 10, 2009
Breaking news
Ndugu wadau wa www.patastories.blogspot.com ninapenda ku-share nanyi kuwa, kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu kamera ya patastories imekumbwa na matatizo ya kiufundi. Hivyo basi natoa masikitiko yangu kuwa speed ya ku-upload itakuwa ndogo kwa siku chache mpaka hapo mambo yatapokaa sawa siku si nyingi.
Niwaombe radhi wale wakiopita kuperuzi kila siku kuwa mambo yatakaa sawa karibuni.
Wenu mdau,
John Mnamba.
Monday, February 9, 2009
Soma hii
Ni habari ya kweli sio hadithi: Ilitokea siku moja wanakijiji walimpeleka mgonjwa wao zahanati ya kijiji. Walipofika zahanati kwa sababu mgonjwa wao alikuwa anaumwa sana wakaandikiwa rufaa ya kwenda katika hospitali ya rufaa (wilayani). Cha kuchekesha na kusikitisha baadhi ya wauguzi (wanakijiji) wa mgonjwa huyo wakamletea mganga wa zahanati hiyo jogoo ili awaahirishie safari ya kwenda hospitali ya wilaya. Yule mganga alishikwa na butwaa na kuwashangaa sana bila majibu. Mganga msimamo wake ulibakia pale pale, alibaki kuwauliza kuthamini utu na huyo jogoo je walifikiria mara mbili au?
Hivi ni vijimambo vya vijijini.
Hivi ni vijimambo vya vijijini.
Subscribe to:
Posts (Atom)












