Sunday, January 25, 2009

Ufahamu kuhusu ugonjwa wa TB

Ili mtu aweze kuugua TB ni lazima awe na mgonjwa aliemuambikiza TB, na yeye awe na upungufu wa kinga mwilini. Upungufu wa kinga mwilini unaweza kusababishwa na maradhi mbalimbali yakiwemo:
Utapiamlo, Kisukari, Surua, UKIMWI na mengineyo.
Pia kinga ya mwili inaweza kupungua ukitumia dawa za kutibu saratani au za kushusha kinga ya mwilini.

Dalili za TB.
Kukohoa mfululizo kwa muda wa wiki mbili (2) au zaidi, na kutoa makohozi safi yaliyochanganyika na damu.
Maumivu ya kifua.
Kutokuwa na hamu ya kula.
Kukonda na kupungua uzito wa mwili na kunakoendelea.
Mwili kunyong’onyea na kuhisi uchovu.
Homa mfululizo.

1 comment:

  1. Aisee that's true man, information delivery.

    ReplyDelete

Be good.