Monday, March 2, 2009

Huyu ndie Jelly fish!


Vyeupe vyeupe vyenye shepu ya duara ndio kiumbe hai wa baharini kwa jina Jelly Fish, moja ya athari zake ambazo mi nimeshadhurika nae ni kwamba akikugusa ni utawashwa kwa maumivu sana. Wanapatikana sana baharini.

Sehemu maalumu ya kuchomea moto maiti!


Eneo hili hutumiwa na watu jamii ya India kuchomea moto maiti za wenzao waliotangulia mbele ya haki, lakini cha kusikitisha vijana waliokosa adabu na heshima wamechora chora ukuta wote.

Ajira na kujiajiri!


Moja ya viwanda vidogo vidogo vya kujipatia ajira.

Friday, February 27, 2009

Mambo ya chips na kuku!


Huwezi amini sehemu hii ndio inatoa chips standard kwa wale tuliozoea chips vumbi.
Ukiachilia mbali chips za mahotelini, kwa wakazi wa Mtwara mjini wanapafahamu hapa.

Thursday, February 26, 2009

Kutoka maktaba!


Nyama ya Tembo ikiwa imabanikwa.
Shea hii yote niliuliza nikaambiwa ni kwa ajili ya wanakijiji wa kijiji husika.

Palikuwa hapatoshi!

4WD inaposhindikana hali ndio huwa hivi.

Vipande vya magazeti...

...vipande hivi nya magazeti vimavirigwa tayari kwa kufungi/kuvirigia bidhaa toka dukani kama sukari nk, cha kusikitisha pamoja na mbinu hii mbadala ya urahisi wa kubeba bidhaa husika ni kwamba wakati vinatayarishwa vilikuwa vipo chini kwenye ardhi. Hivyo kiafya inakuwa haijakidhi kisawa sawa kwa namna moja ama nyingine.