Link ifuatayo chini inaweza kukupa idea fulani kuhusu gari yako...
Saturday, January 31, 2009
Teknolojia...
Teknolojia moja inapoipiku ingine huua kwa namna moja ama soko wa iliyopita, pichani ni kifaa chenye uwezo kama flash disk kenye uwezo wa kuhifadhi na kusikiliza mziki uwapo garini. Ni teknolojia nzuri sikata, hasa kwa barabara za vijijini ambapo CD kwenye kashkash za rafu road inakata kuimba. Wanasema Mchina huyo bwana.
Friday, January 30, 2009
Cheka Kiafya!!
Kuna sehemu moja Mkoani Mtwara inaitwa Nakapanya na ingine inaitwa Nanguruwe, hii ni kweli na ucheke kiafya tu sio sana. Kuna dada mmoja wakati mahojiano yakiendelea kuhusu maisha yake nk, nk, ilifika kipindi katika maelezo yake ilikuwa hivi:
...mimi niliolewa Nakapanya nikaachika nikaenda kuishi Nanguruwe...
Yaani akimaanisha aliwahi ishi maisha ya ndoa Nakapanya na baadae akaenda kuishi Nanguruwe.
Ni story ya kweli si ya kutunga.
Kiafya tafadhali!
Hali halisi kipindi cha mvua...
Watoto hawa nimewakuta wakicheza kwenye maji yaliyotuama ya mvua. Yawezekana shida ya maji vijijini hufanya mpaka hali kama hii ikitokea watoto hawa husherekea. Na wazazi wao sio kwamba walikuwa mbali na watoto hao? Hapana.
Huyu ndie nisema kama kwenye swimming pool basi ndio yupo deep.
Vijimamboz hivyo na patastories.
Huyu ndie nisema kama kwenye swimming pool basi ndio yupo deep.
Vijimamboz hivyo na patastories.
Ukweli kuhusu Prison Break
Prison Break
Ukweli kuhusu Prison Break, imezoeleka masikioni na machoni mwa wengi kuona mitaani Prison Break inapatikana mpaka season eight (8). Hii nathibitisha wazi kuwa Prison Break kihalisia haijafika season eight (8). Hizi mnazoziona mitani ni Episodes tu toka season halali season four (4).
Kwa wanaofuatilia kwa makini watajua ninamaanisha nini. Ukweli ni kwamba kibiashara tu ili kupata pesa wadau Fulani fulani ili wasilale njaa ndio wameamua kuikata kata vipande “episodes” hizo na kuzigawanya katika mafungu wayajuayo wenyewe na kuyaita “season Fulani mpaka Fulani. Ukweli unabaki pale pale kuwa wananchi wamekuwa wakinunua season moja mara nne zaidi bila wao kujua. Ila kutokana na utamu wa sinema yenyewe then watu kwao ni sawa tu bora kuona.
Ilikuwa ni katika kupeana dodoso tu habari ndio hiyo ipo nje nje.

Thursday, January 29, 2009
Ukisikia mkonge ndio huu!!!
Kama inavyoonekana pichani, mkonge wa moja ya gari za kazi Land Cruiser ukiwa umechomewa kwa lengo kuubwa la kupambana na vibaka. Inasemekana gari kama hiyo pindi (Mfano) ipatapo ajali wale wapenda kung'oa vifaa hukimbilia huo mkonge. Habari zinasema kwamba unagharama kuubwa sana ndio sababu ya vibaka kuwinda ulaji huo wanaojua/fahamu magari wanaelewa hilo.
Nauli!
Inasemekana kuwa kwa baadhi ya magari almaarufu makenta ama malori yabebayo abiria yanayofanya safari zake kwenda Tunduru kupitia njia ya Mtwara wanawake ndio hulipa nauli kubwa, hili nikauliza na kujibiwa kuwa baadhi ya makenta/malori hayo ni vimeo (Mabovu) hivyo linapohitaji msaada wa kulisumkuma liwake wanaume ndio wanashughulika. Swali je kwa mwanaume akitaka kulipa nauli kubwa kidogo na yeye atakubaliwa?
Wednesday, January 28, 2009
PPF tower ya mchwa!
Ghorofa hili limejengwa na mchwa, wadudu hawa wanaushirikiano wa hali ya juu. Siku moja nilibahatika kupita na kuingia nyumba moja kijini na kukuta pamebomolewa kitu mfano wa huo pichani. Nikauliza wakasema ni mchwa hao, na kubomoa tu hakusaidiii maana wanajenga tena, watalamu husema mpaka apatikane malkia wao mchwa ndio wanahama na wenyewe kazi ambayo sio nyepesi kama unavyoifikiria.
Tuesday, January 27, 2009
Video show...
Uwapo kijijini na ukashuhudia kasha la Video kaseti likining'inia kwa mtindo huo linamaanisha kuwa nido picha itayoonyeshwa kenye kaukumbi husika kwa kiingilio cha kati ya shilingi hamsini na mia. Na kikubwa zaidi picha hizo kuwazanakuwa na mtu anaetafsiri iwe ya kihindi nk
Nakushauri siku moja ukiwa kijijini ingia sehemu kama hizo usikie yanayozungummzwa na kutafsiriwa ufe mbavu.
Subscribe to:
Posts (Atom)