Saturday, February 7, 2009

Kutoka Maktaba!!

Sio vita, ni sherehe za kimila ambazo hufanyika kila mwaka huku visiwani (Zanzibar).
Pichani moja ya walioenda kushuhudia aliamua kujitosa kukamilisha shughuli hiyo.

Wakati wa kupeana kipondo huwa wanatumia migomba na si mmea mwingie wowote kuepusha majeruhi wakati wa sherehe kama hizo almaarufu kama "Mwaka koga"

Vijana wakionyeshana maujuzi wakati wa kuchapana na silaha Mgomba.

Hapa ni mchakamchaka kabla ya shughuli yenyewe kuanza, huwa wanaimba nyimbo ambazo hata ukizi-edit bado hazifai katika jamii yetu ya Mtanzania mstaarabu kama wewe.

Wakina mama nao huwa hawakubali kuachwa nyuma.
Mwaka huu sitobahatika kuwepo eneo husika nikupatie vionjo.


No comments:

Post a Comment

Be good.