Ukiachilia mbali chips za mahotelini, kwa wakazi wa Mtwara mjini wanapafahamu hapa.
Friday, February 27, 2009
Thursday, February 26, 2009
Vipande vya magazeti...
...vipande hivi nya magazeti vimavirigwa tayari kwa kufungi/kuvirigia bidhaa toka dukani kama sukari nk, cha kusikitisha pamoja na mbinu hii mbadala ya urahisi wa kubeba bidhaa husika ni kwamba wakati vinatayarishwa vilikuwa vipo chini kwenye ardhi. Hivyo kiafya inakuwa haijakidhi kisawa sawa kwa namna moja ama nyingine.
Wednesday, February 25, 2009
Tuesday, February 24, 2009
Kutoka ushauri na maoni mbali mbali
Nianze kwa kuwashukuru mnao nipatia muda wenu na kupita katika blog yangu kuperuzi hili na lile. Lingine lililoniofanya niandike ujumbe huu ni kwamba, baadhi ya wadau kwa namna moja ama nyingine wameomba kuwepo pia picha zinazogusa/zungumzia mazingira na mila pamoja na desturi za huko vijijini nipitako kila kukicha. Jibu nililokuwa nalo la haraka haraka la kueleweka ni kwamba:
Mimi binafsi ni mfanyakazi wa NGO fulani hivyo kupata picha za mila na desturi nk inakuwa ngumu kwa sababu muda wangu mwingi nakuwa bize na kazi inayonipatia ugali.
Pili, sitoweza tumia muda wa kazi kwa kufanya mambo yangu binafsi kwani kazi ni kitu ninachokiheshimu kuliko ugali ninaokula.
Tatu, picha unazozipata (vionjo) unavyovipata ni matokea ya yale ambayo kwa namna moja ama nyingingine nimekuwa nikikutana nayo wakati nikiwa eneo husika, hivyo basi niwaombe radhi kama kuna machache nitakuwa nakunyima kutoka pande za vijijini.
Pamoja na hayo nakutakia siku njema yenye baraka.
Pia nashukuru kama umenielewa maneno yangu.
Wako Mdau.
Taswira
Hiyo myeusi ni mipira itumikayo sana kufungia bidhaa/kitu/mzigo fulani kwa watumiaji wa baiskeli, hali hii ni kutokana ya kwamba kijijini baiskeli ndio njia rahisi ya usafiri wa haraka haraka.
Monday, February 23, 2009
Sunday, February 22, 2009
Saturday, February 21, 2009
Majibu ya post hii ya 23/1/2009 ni haya hapo chini.
Nimebahatika kuona pindi niwapo katika mizunguko yango ya kila siku vijijini kwa gari na kushuhudia nyuma baada ya kupita kwa baadhi ya wanavijiji huchukua wanao wadogo na kwenda kuwakanyagisha zilipoacha/pita alama za matairi ya gari. Nimeshindwa kujua bado mpaka sasa ni nini maana yake!?Wewe una ufahamu wowote juu ya hili?
............................................
Jibu nililolipata ni kwamba,
Wanafanya hivyo kwa mtoto ambae hajaanza kutembea iwe kama kum-wish atembee haraka kwa siku za usoni.
Ndivyo nilivyoambiwa sasa kama ni kweli au la! Hayo ndio majibu
Siri na raha ya kijijini ni...
Hali kama hii huwezi linganisha na wenye nyumba mjini kwa baadhi ya maeneo ya hali ya juu.
Wanasema maisha popote bwana bora kuridhika na ulichonacho.
Friday, February 20, 2009
Subscribe to:
Posts (Atom)